1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiVatican

Papa Leo XIV kufanya ziara katika mataifa manne ya Afrika

26 Februari 2026

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV anatarajia mwezi Aprili kufanya ziara katika mataifa manne ya Afrika ikiwa ni pamoja na Algeria, Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Leo XIV akiwahutubia wauminiPicha: Alessandra Tarantino/AP Photo/picture alliance

Kiongozi huyo wa kidini atautembelea mji mkuu wa Algeria na eneo la Annaba kuanzia Aprili 13 hadi 15, ikiwa ni ziara ya kwanza katika taifa hilo la kiislamu la Afrika Kaskazini.

Akiwa huko Cameroon na Angola,  Papa Leo anatarajia kutoa wito wa amani  na mazungumzo ya kijamii kufuatia migogoro ya muda mrefu ya makundi yanayotaka kujitenga na mbayo yamekuwa yakisababisha vifo vya raia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW