Maelfu ya raia kushiriki misa na Papa Leo XIV mjini Douala
17 Aprili 2026
Matangazo
Tukio hilo limewakusanya karibu watu laki sita kwenye mitaa inayouzunguka uwanja wa Japoma watakaposikiliza hotuba ya Papa. Idadi kubwa ya watu wenye shauku ya kumsikia na kumuona kiongozi huyo waliingia katika viwanja hivyo tangu jana kwa ajili ya tukio hilo.
Papa Leo na ujumbe wa amani kwa Afrika
Awali siku ya Alhamisi, Papa Leo XIV alitoa ujumbe mzito mjini Bamenda kulikoathiriwa na vita ambako alitoa wito wa mabadiliko na kuithamini amani. Papa Leo amewakosoa pia wageni wanaoinyonya Afrika na kuongeza kuwa wanachangia umasikini na ukosefu wa maendeleo barani humo.