1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Leo ziarani Uturuki kwa mazungumzo na Erdogan

27 Novemba 2025

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIV amewasili nchini Uturuki atakapokutana na kufanya mazungumzo na Rais wa taifa hilo Recep Tayyip Erdogan. Baada ya Uturuki, ataelekea Lebanon Jumapili.

Papa Leo XIV katika hafla ya kumpokea alipowasili Uturuki Novemba 27, 2025
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Leo XIVPicha: Yara Nardi/REUTERS

Katika ziara yake hiyo ya kwanza nje ya kimataifa Papa Leo anatarajiwa kuhudhuria kumbukumbu muhimu ya madhehebu ya Orthodox na kutoa ujumbe wa amani katika juhudi za kuleta amani katika maeneo yenye mizozo yakiwemo Ukraine na Mashariki ya Kati.

Papa Leo kuhudhuria mikutano ya kidini Istanbul

Baada ya kukutana na Rais Erdogan mjini Ankara, Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani ataelekea Istanbul kwa ajili ya mikutano ya kidini na kisha ataelekea Lebanon Jumapili.

Kwa Vatican, utamaduni wa uvumilivu wa kidini wa Lebanon katika Mashariki ya Kati ni ngome kwa Wakristo  wa kanda hiyo hasa baada ya miaka mingi ya migogoro na vita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW