Jeshi la Misri limeyagundua mabaki ya ndege ya shirika la EgyptAir katika bahari ya Meditarrania, msichana wa pili Kati ya waliotekwa na Boko Haram mjini Chibok Nigeria akombolewa na jeshi la nchi hiyo, mwanasiasa wa upinzani DRC Moise Katumbi afunguliwa mashitaka, Taiwan yamuapisha rais wake wa kwanza mwanamke, na Pizza ndefu zaidi yenye urefu wa maili moja yatengenezwa Italia.