SiasaParaguay
Paraguay yaipigia chapuo Taiwan kujiunga Umoja wa Mataifa
20 Septemba 2023![Rais Santiago Pena wa Paraguay (kushoto) na rais Tsai Ing-wen wa Taiwan](https://static.dw.com/image/66196894_800.webp)
Matangazo
Pena ametoa matashi hayo katika hotuba yake mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa aliyoitoa usiku wa kuamkia leo.
Kiongozi huyo wa Paraguay, taifa pekee la Amerika ya Kusini ambalo bado linaitambua Taiwan kuwa nchi kamili, amesema ni muhimu kwa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kulitafutia jawabu suala la hadhi ya Taiwan.
Kisiwa hicho chenye utawala wake wa ndani kilizuiwa kuchukua kiti kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika yake mwaka 1971 baada ya chombo hicho kuitambua Jamhuri ya Umma wa China kuwa mwakilishi rasmi wa China ndani ya umoja huo.
China inaizingatia Taiwan kuwa sehemu ya milki yake licha ya kisiwa hicho kuipinga vikali sera hiyo.