1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS Hali ya tahadhari yatangazwa nchini Ufaransa

14 Julai 2005

Polisi nchini Ufaransa imewekwa katika hali ya tahadhari kabla kuanza maadhimisho ya siku ya Bastille hii leo. Maofisa yapata 5,000 watapelekwa kwenye maeneo mbalimbali ya mji wa Paris kulinda usalama.

Watu watakaokusanyika kwa sherehe hizo wameshauriwa waache mikoba yao nyumbani kama tahadhari. Ufaransa ilitangaza hali ya hatari katika kiwango cha pili cha rangi nyekundu kufuatia mashambulio ya mabomu mjini London.