1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Kansela Gerhard Schroeder atakuwa kiongozi wa kwanza ...

2 Januari 2004
wa kijerumani kuhuhuria sherehe za kuadhimisha siku ya kuteremka wanajeshi mwaka 1944. Msemaji wa serikali mjini Berlin amethibitisha kansela Schroeder amekubalia mualiko wa rais Jacques Chirac wa Ufaransa kuhudhuria sherehe hizo Normandy mwezi Juni. Juni sita mwaka 1944, majeshi ya muungano yalianzisha kampeni dhidi ya Wanazi yalipowasili pwani ya Normandy. Siku hii kila mwaka inatukuzwa na wanasiasa na wakongwe wa kivita katika zile sehemu walizoteremkia wanajeshi wa muungano wakati wa vita vya pili vya dunia.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW