1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris: Kiongozi wa upinzani wa Ujerumani, Bibi Angela Merkel, amefanya mazungumzo na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa

19 Julai 2005

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Ujerumani, Bibi Angela Merkel, ameusifu uhusiano baina ya Ujerumani na Ufaransa na kuuita kuwa ni muhimu, na jambo hilo halitegemei matokeo ya uchaguzi katika nchi hizo mbili. Aliyasema hayo baada ya kukutana na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa katika Kasri la Elysee. Bibi Merkel alisema nchi zote mbili zinataka Ulaya ilioungana. Hatua za kisiasa ndani ya Jumuiya ya Ulaya zinafaa zipigwe jeki na injini ya pamoja ya Ujerumani na Ufaransa, na jambo hilo, lakini, liko wazi kwa nchi nyingine wanachama. Kabla ya ziara hiyo, Bibi Merkel alilauamu mashikamano makubwa baina ya Kansela Gerhard Schroader wa Ujerumani na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa kuwa ni mzigo kwa washirika wadogo katika Jumuiya ya Ulaya.