1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Mgomo wa taifa Ufaransa waathiri huduma

11 Machi 2005

Mgomo wa taifa nchini Ufaransa umevuruga vibaya huduma za treni na reli za chini ya ardhi hapo jana pamoja na kuchelewesha safari kadhaa za ndege.

Vyama vya wafanyakazi vimetowa wito wa migomo hiyo kupinga mipango ya serikali ya kuregeza sheria juu ya masaa 35 ya wiki ya kazi.Migomo hiyo imefanyika wakati wakaguzi kutoka Kamati ya Kimataifa ya Olympik wakiwa ziarani mjini Paris kutathmini uwezo wa mji huo unaowania kuandaa mashindano ya Olympik ya mwaka 2012.