PARIS: Rais wa Burundi Domitien Ndayizeye amakutana na ...
17 Januari 2004Matangazo
mwenzake wa Ufaransa Jacques Chirac wakati akiwa na ziara mjini Paris kama ni sehemu ya ziara yake ya Ulaya ya kutafuta misaada wa kimataifa kwa ajili ya nchi yake. Chirac alisema Ufaransa itachukua juhudi za hali ya juu kuisaidia Burundi. Ndayizeye aliwasili Paris jana akitokea Brussels ambako wafadhili walimuahidi EURO kama Billioni moja kama msaada kuifanya Burundi ijisaidie kufuatia miaka zaidi ya 10 ya vita vya kiraia nchini. Ufaransa inalenga mambo mawili, kusaidia kuboresha uhusiano baina ya Burundi na taasisi za kifedha za kimataifa, na misaada kwa wakimbizi wa dola hiyo ya Maziwa Makuu.