1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris Saint German mabingwa wa UEFA Super Cup

13 Agosti 2026

Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi kutoka Somalia Omar Artan ambaye simulizi yake ya kukataliwa kuingia Marekani kushiriki Kombe la Dunia iliwagusa wengi.

UEFA Super Cup 2026 | PSG vs. Aston Villa | PSG-
Mabingwa wa UEFA Super Cup, Paris Saint German Picha: Franck Fife/AFP

Klabu ya soka ya Paris Saint German kwa mara nyingine imetetea ubingwa wa Kombe la UEFA Super Cup usiku wa kuamkia leo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Aston Villa ya England.

PSG ambayo imekuwa katika ubora mkubwa sasa imefikisha makombe manne ya Ulaya ndani ya misimu miwili. Mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya na mawili ya UEFA super Cup.

Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi kutoka Somalia Omar Artan ambaye simulizi yake ya kukataliwa kuingia Marekani kushiriki Kombe la Dunia iliwagusa wengi.

Kwingineko huko Tanzania, Klabu ya Yanga imeibuka na ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuwafumua watani wao wa jadi Simba 1-0.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW