1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Sarkozy azinduwa kampeni ya Urais

15 Januari 2007
Kansela Merkel katika bunge la Umoja wa Ulaya
Kansela Merkel katika bunge la Umoja wa UlayaPicha: AP

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameanzisha kampeni yake ya kuwania Urais katika mkutano wa chama uliofana mjini Paris hapo jana kwa wito wa kuwataka wapiga kura wa imani zote wamchaguwe awe rais wa watu.

Katika hotuba kwa wanachama 80,000 wa chama tawala cha Union for Popular Movement Sarkozy ameelezea ilani yake kwa mapana akisisitiza thamani ya kazi na kuahidi kurudisha mamlaka yenye uwezo wa kisheria kutekeleza mambo na heshima pamoja na kuunda jamii ya wajibu na haki.

Sarkozy mwenye umri wa miaka 51 mtoto wa mhamiaji wa Hungary ni mwanasia pekee ambaye uchunguzi wa kura za maoni unasema anaweza kumshinda mgombea wa Kisoshalisti Segolene Royal ambaye anatarajiwa kuchukuwa nafasi ya Rais Jacques Chirac ili kuja kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Ufaransa.

Uchaguzi huo mkuu wa Ufaransa umepangwa kufanyika mwezi wa April.