1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Ufaransa kufuata nyayo za Ujerumani

14 Septemba 2007

Waziri Mkuu wa Ufaransa Francois Fillon ameitaka Ufaransa kufuta nyayo za Ujerumani katika kufanya mageuzi makubwa.

Katika makala yanayotazamiwa kuchapishwa leo hii katika gazeti la Ujerumani la Frankfurter Allgemeine na Le Figaro la Ufaransa Fillon anasema Ufaransa inahitaji kuangalia mbele zaidi na kuwa na malengo makubwa.Waziri Mkuu huyo wa Ufaransa leo anatazamiwa kuhutubia mkutano wa viongozi wa biashara katika mji wa kitalii wa Evian kwenye milima ya Alpine.

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy ameahidi kuichochea Ufaransa katika ukuaji wa haraka wa uchumi kwa kufanya mageuzi makubwa ya kiuchumi.

Halmashauri ya Umoja wa Ulaya imetabiri wiki hii kwamba uchumi wa Ufaransa ambao ni wa pili kwa ukubwa katika eneo la Ulaya utakuwa kwa kiwango cha chini ya asilimia mbili mwaka huu.