1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris: Ufaransa yainyoesha mkono Marekani

13 Novemba 2003
Ufaransa inataka kuisaidia Marekani katika "mzozo wake wa kuhuzunisha" nchini Iraq, waziri wa mambo ya nje Dominique de Villepin alisema hii leo, lakini inaamini kwamba jambo muhimu kabisa ni kukabidhiwa upesi Wairaki madaraka ya kiutawala. "Hii leo tutayari kujumuika katika mkutano wowote ule au mashauriano yoyote yale. Tunawanyoshea mkono marafiki zetu wa Marekani, kwa sababu changamoto inatuathiri sisi sote. Suala linalohusika ni usalama wa dunia," aliiambia Europe 1 Redio. Alisema kwamba Rais Bush anaweza kutaraji mshikamano wa mawazo na ujasiri pamoja na Ufaransa. Ufaransa ni rafiki na mshirika wa Marekani.