1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ufaransa yapiga marufuku mashirika ya ndege yasitumie viwanja vyake

29 Agosti 2005

Maofisa wanaongoza safari za ndege nchini Ufaransa wametoa orodha ya majina ya makampuni ya ndege ambayo hayana ruhusa tena ya kutumia uwanja wa ndege wowote nchini humo kwa sababu za usalama.

Orodha hiyo inayajumulisha makampuni ya Korea Kazkazini, Virgin Islands kutoka Marekani, Liberia, Thailand na Msumbiji. Hatua hii inaifanya Ufaransa kuwa taifa la tatu barani Ulaya kuchapisha orodha kama hiyo baada ya Uingereza na Sweden.