1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Ufaransa yatingishwa na mgomo wa siku moja

5 Oktoba 2005

Ufaransa imekumbwa na mgomo wa siku moja ulioitishwa na wafanyakazi wa huduma za usafiri za taifa,walimu na watumishi wengine wa sekta za serikali.

Maafisa wa vyama vya wafanyakazi wamesema takriban watu milioni moja hawakwenda makazini hapo jana.Wagomaji walikuwa wakilalamikia sera za ajira na uchumi za serikali ya mrengo wa kulia wa wastani ambazo zimepelekea kuwepo kwa kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira na kushuka kwa hali ya maisha.

Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa serikali hiyo kukabiliwa na hatua nzito kama hiyo tokea Dominique de Villepin awe waziri mkuu miezi minne iliopita.

Vyama vya wafanya kazi vimetishia kurudia tena mgomo wao venginevyo madai yao ya kuongezewa mishahara na usalama wa kazini yanatimizwa.