1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Ujerumani na Ufaransa zashinikiza kuridhiwa katiba ya Ulaya

11 Juni 2005

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani na Rais Jacques Chirac wa Ufaransa wametowa wito wa pamoja kwa nchi kuendelea kuidhinisha Katiba ya Umoja wa Ulaya licha ya katiba hiyo kukataliwa katika kura za maoni nchini Ufaransa na Uholanzi pamoja na kuahirishwa kwa kura hiyo nchini Uingereza.

Schroeder akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mjini Paris amekanusha kwamba katiba hiyo imekufa. Juu ya suala la bajeti ya Umoja wa Ulaya yenye utata Schroeder amesema nchi zote mbili Ujerumani na Ufaransa ziko tayari kufikia muafaka lakini ameongeza kusema kwamba nchi nyingine pia nazo inabidi zikubali kuridhia.Chirac ameitaka Uingereza iachane na punguzo lake la bei la mabilioni ya uero kwa ajili ya kulipa fedha taslim.

Hata hivyo Uingereza inasema haitojadili suala hilo bila ya kufanya mapitio makubwa kwa matumizi ya Umoja wa Ulaya.