1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Wasi wasi kuhusu wahamiaji nchini Morocco

8 Oktoba 2005

Shirika la misaada la MSF limesema wakuu wa Kimorocco wamewaacha jangwani,si chini ya wahamiaji 500 wa Kiafrika bila ya chakula au maji karibu na Algeria.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan ameeleza wasi wasi kuhusu mgogoro wa wakimbizi katika Afrika ya Kaskazini na kusema kuwa hali ya mambo ni tete.Kwa wakati huo huo Mkuu wa Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Antonio Guterres amesema,Shirika hilo linajadiliana na wakuu wa Hispania na Morocco kuhakikisha kuwa wale wanaojaribu kuingia ardhi ya Hispania wanatazamwa kihaki na kiutu.