1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Waziri mkuu wa Chad afariki dunia

23 Februari 2007

Waziri mkuu wa Chad. Pascal Yoadimnadji, amefariki dunia mjini Paris, Ufaransa. Kiongozi huyo alisafirishwa mjini humo kwa matibabu ya dharura baada ya kupata mshuto wa moyo.

Pascal, mwenye umri wa miaka 56, na aliyekuwa zamani waziri wa kilimo, aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa Chad mnamo mwezi Februari mwaka wa 2005 na rais Iddris Deby, aliyechukua madaraka wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka wa 1990.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW