1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Ajali nyingine ya moto yaua Waafrika saba Ufaransa.

30 Agosti 2005

Ajali nyingine ya moto imetokea mjini Paris,katika jengo wanalosihi wahamiaji wa Kiafrika na watu saba wamekufa kufuatia moto huo.

Wazima moto wameeleza kuwa kiasi cha watu 14 wengine wamejeruhiwa,watatu wakiwa katika hali mbaya.

Ajali hii imetokea baada ya kutokea ajali nyingine ya moto chini ya wiki moja,baada ya jengo jingine kuwaka moto mjini Paris na kusababisha Waafrika 17 kupoteza maisha yao.