1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris.Chirac aahidi kufufua mazungumzo ya amani kati ya Palestina na Israel.

4 Septemba 2006

Rais wa Ufaransa Jacques Chirac amefanya mazungumzo hii leo na Ahmed Korei, mjumbe maalum kutoka kwa rais wa Palestina Mahmud Abbas, na kutaka kufanyika kwa mazungumzo mapya kati ya nchi yake na Israel ili kuleta hali ya amani.

Kwa mujibu wa maneno yaliyotolewa na ofisi ya rais yamesema kuwa, Chirac amemtaka Korei kumuelezea rais Mahmud Abbas msimamo wa Ufaransa wa kumuunga mkono katika juhudi za kutafuta amani.

Aidha Chirac ameongeza kwa kusema kuwa kutokana na umoja wa wananchi wa Ufaransa kwa ndugu zao wa Palestina katika matatizo yanayowakabili , nchi hiyo itahakikisha inafanya juhudi zote ili kuona mazungumzo hayo ya kutafuta amani yanafanyika.

Mwishoni mwa wiki rais Chirac alitaka kufanyika kwa mkutano wa mashariki ya kati akizitaja pande nne ambazo ni Marekani, Urusi, Umoja wa nchi za Ulaya na Umoja wa Mataifa kwa madhumuni ya kurejesha upya mazungumzo ya amani.