1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris:Chirac akutana na Schröder:

9 Desemba 2003
Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani na Rais Jacque Chirac wa Ufaransa wamezungumzia kuhusu kutofanyiwa marekebisho makubwa muswada wa katiba ya Umoja wa Ulaya wakati wa mkutano mkuu ujao wa Viongozi wa Umoja huo. Rais Chirac, baada ya kuzungumza na Kansela Schröder mjini Paris, amesema kuwa tofauti huenda zikatokea kuhusu muswada huo lakini lazima Viongozi waafikiane. Kansela Schröder naye amesema kuwa lengo kubwa ni kuafikiana na ndiyo maana anakwenda Brussels akiwa na matumaini makubwa. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Joschka Fischer, kabla ya hapo amewaomba Viongozi wa nchi wanachama na wale wanaotaka kujiunga na Umoja wa Ulaya kutoweka mbele maslahi ya nchi zao. Masuala yanayoleta mivutano ni haki ya kupiga kura katika maamuzi ya Baraza la Mawaziri na muundo wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW