1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Je katiba ya umoja wa Ulaya ndo imeangamia?

30 Mei 2005

Wafaransa wameipinga kabisa katiba ya umoja wa Ulaya katika kura ya maoni iliyopigwa hapo jana.

Huku takriban kura zote zikiwa zimehesabiwa asilimia 55 imeipinga katiba hiyo mpya ya Umoja wa Ulaya,iliyoundwa kwa ajili ya kurahisisha upitishaji wa maamuzi katika Umoja huo kufuatia kuongezeka kwa wanachama wake hapo mwaka uliopita.

Akijibu kwa haraka kuhusu uamuzi wa wafaransa rais Jack Chirac,kupitia televisheni ya taifa aliwaonya wananchi wake kwamba hatua hiyo itasababisha hali ngumu kwa nchi hiyo katika kutetea manufaa yake kwenye umoja wa Ulaya .

Katiba hiyo sasa imebakia katika hali ya ati ati kwani haiwezi kufanya kazi hadi ikubalike na mataifa yote 25 wanachama wa Umoja huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW