1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Libya kulipa fidia wahanga wa ndege ya Ufaransa

9 Januari 2004
Familia za watu 170 waliouwawa kutokana na kuripuliwa kwa ndege ya Ufaransa kunakolaumiwa kuwa kumetekelezwa na Libya wamekubali makubaliano yaliokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu ya kulipwa fidia na serikali ya Tripoli.

Afisa wa serikali ya Ufaransa amesema Libya italipa dola milioni 170 kwa wahanga wa familia ya ndege ya shirika la ndege la Ufaransa UTA ilioripuliwa juu ya anga ya Niger hapo mwaka 1989.

Hata hivyo malipo hayo ni pungufu sana ikilinganishwa na makubaliano ya malipo ya fidia ya dola bilioni 2.7 yaliofikiwa mwaka jana kati ya Libya na wahanga wa familia ya ndege ya shirika la ndege la Marekani Pan Am iliyoripuliwa juu ya anga ya Lockerbie Scotland hapo mwaka 1988.