1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Makomandoo wa Ufaransa waikomboa meli iliyokuwa imetekwa.

28 Septemba 2005

Vikosi vya jeshi la Ufaransa,vimeivamia na kuikamata tena meli iliyokuwa inashikiliwa na wanachama wa vyama vya wafanyakazi.Kiasi cha makomandoo 50 wa kikosi maalum,waliteremshwa kwa helikopta katika daraja la Pascal Paoli,wakiwa katika jitahada za kuingia katika bandari ya Bastia.

Meli hiyo ilishikiliwa mjini Marseille tangu jana na kikundi cha wanaharakati wa vyama vya wafanyakazi,wakipinga mipango ya serikali ya kubinafsisha kampuni inayosimamia vivuko ya SNCM ambayo inakabiliwa na madeni.

Wanaharakati hao wanahofia kuuziwa kampuni binafsi,kunaweza kusababisha watu kwa mamia kukosa ajira.

Kampuni ya SNCM huduma zake zinafika hadi Corsica,Algeria na Tunisia.