1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Raia wa nje kufukuzwa Ufaransa

10 Novemba 2005

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa bwana Nicolas Sarkozy ametoa amri ya kufukuzwa nchini kwa raia wote wa nchi za nje waliopatikana na hatia ya kushiriki katika ghasia za mjini Paris.

Bwana Sarkozy ameliambia bunge kwamba raia wa nje 120 wamepatikana na hatia hiyo na kwamba watafukuzwa nchini Ufaransa mara moja.

Wakati huo huo habari zinasema kwamba,kwa jumla hali imeendelea kuwa tulivu .