1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS:Ufaransa kupewa msaada na Umoja wa Ulaya

14 Novemba 2005

Kwa usiku wa 18 kwa mfululizo ghasia na fujo za kuchoma mali zimeendelea nchini Ufaransa.Mara nyingine tena magari mia kadhaa yalitiwa moto na polisi wamewakamata watu 112.Hali ya machafuko ikiendelea nchini Ufaransa,Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya,Jose Manuel Barroso amependekeza kuipa Ufaransa msaada wa Euro milioni 50 kutenzua matatizo ya ajira na ya kijamii katika maeneo ya machafuko.Wakati wa ziara yake mjini Paris, Barroso alisema matatizo makuu ni ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana na kuwajumuisha wahamiaji.Akaeleza kuwa hayo ni matatizo yanayokabiliwa na miji mingi ya Ulaya.Ghasia za usiku wa Jumapili zilikuwa mbaya zaidi katika miji ya Lyon,Toulouse na Paris amabako magari 271 yalitiwa moto.Tangu ghasia hizo kuanza wiki mbili zilizopita,hasara ya mali iliyopatikana inakadiriwa kuwa zaidi ya Euro milioni 240.Leo serikali ya Ufaransa inakutana kujadiliana juu ya mswada wa kurefusha amri ya kuzuia watu kotuka nje nyakati za usiku na mamlaka ya kupambana na hali za dharura.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW