1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS.Ujerumani na Ufaransa zataka katiba ya ulaya iendelee

10 Juni 2005

Kansela Gerhard Schröder wa Ujerumani na rais Jacque Chirac wa Ufaransa wametoa wito wa kuendelezwa kwa katiba ya umoja wa ulaya licha ya katiba hiyo kukataliwa katika kura ya maoni na Ufaransa na Uholanzi na kubadili nia ya kuendelea na kura hiyo huko Uingereza.

Bwana Schröder aliyasema hayo wakiwa pamoja na rais Chirac na akasisitiza kuwa ni mapema mno kuitumbukiza katiba ya umoja wa ulaya katika kaburi la sahau.

Viongozi hao wemesema pia Ufaransa na Ujerumani ziko tayari kuafikia maridhiano juu ya bajeti ya umoja wa ulaya kabla ya mkutano wa umoja huo utakao anza wiki ijayo hata hivyo hakufafanua zaidi juu ya maridhiano hayo.