1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Pasaka ya Orthodox nchini Ukraine yagubikwa na mashambulizi

16 Aprili 2023

Mapigano yameendelea kushuhudiwa nchini Ukraine katika mji wa kusini mwa nchi hiyo wa Mykolayiv usiku wa kuamkia leo licha ya maadhimisho ya sikuku ya Pasaka kwa waumini wa madhehebu ya Orthodox.

Pichani ni kasisi Yuriv Potykun akimwaga maji ya baraka kwenye mahandaki ya wanajeshi wa Ukraine kabla ya sikukuu ya Pasaka kwa waOrthodox.
Bado kunashuhudiwa mashambulizi makali nchini Ukraine na hasa katika mji wa Bakhmut. Picha: Sergey Bobok/AFP/Getty Images

Mapigano hayo ya mapema leo yamesababisha vifo vya watoto wawili, hii ikiwa ni kulingana na gavana wa kijeshi Vitaly Kim.

Katika jimbo la Zaporizhzhya, mkuu wa utawala wa kijeshi Yuri Malashko pia amearifu kuhusu shambulizi la Urusi lililoharibu kanisa, kwa lengo la kuvuruga shughuli za ibada zilizotakiwa kufanyika leo.

Soma Zaidi: Ukraine: Urusi yadai kusonga mbele katika mji wa Bakhmut

Katika hatua nyingine, katika mji wa mashariki wa Sloviansk, shambulizi la roketi lilipiga jengo la makazi ya watu siku ya Ijumaa na kazi ya kuwaokoa wakazi walionasa chini ya vifusi inaendelea, wakati kukiripotiwa watu 11 kuuawa katika shambulizi hilo.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika ujumbe wa sikukuu hiyo, amewahamasisha wanajeshi wake kuendelea kuamini kwamba watavishinda vita hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW