Patrice Motsepe apinga madai ya CAF kupokea rushwa
19 Machi 2026
Kamati ya rufaa ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) iliamua Jumanne kuipatia ubingwa Morocco baada ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani kwa hasira wakipinga adhabu ya penalti. Baadaye walirejea na kushinda mechi hiyo katika muda wa nyongeza, lakini ushindi huo sasa umefutwa.
Senegal ilikasirika sana, ikisema itakata rufaa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo (CAS), na hata serikali jijini Dakar ikaingilia na kuihusisha CAF na ‘ufisadi.'
Motsepe alitoa tamko kwa njia ya video Jumatano usiku akikataa madai yoyote ya makosa upande wa CAF, akisema kuwa majaji na wanasheria mashuhuri kutoka Afrika walihusishwa katika kamati ya rufaa. Aidha rais huyo pia alikemea vikali vitendo vya Senegal wakati wa fainali akisema vinadumisha dhana potofu kuhusu soka la Afrika.