1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pendekezo la kumaliza vita Gaza laitikisa serikali ya Israel

3 Juni 2024

Mshirika wa muungano wa serikali ya mrengo mkali wa kulia nchini Israel ametishia kwa mara nyingine kujitoa kwenye serikali, iwapo waziri mkuu Netanyahu atamaliza vita Ukanda wa Gaza.

Israel Jerusalem | Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel Itamar Ben-Gvir
Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel Itamar Ben-GvirPicha: Debbie Hill/UPI Photo/IMAGO

Mwanasiasa huyo ambaye ni waziri wa Usalama wa Taifa Itamar Ben-Gvir amemshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu hii leo kwa kujaribu "kuyaficha" yaliyomo katika makubaliano ya kumalizavita vya Gaza yaliyopendekezwa na Rais wa Marekani Joe Biden

Ameziambia pande pinzani bungeni kwamba Netanyahu alimwalika kwenda kusoma pendekezo hilo, lakini wasaidizi wa kiongozi huyo walishindwa mara mbili kumpa waraka huo na kusisitiza, mpango wowote ni lazima ulenge kuliangamiza kundi la Hamas.

Mapema, Netanyahu alisema lengo kuu la vita vya Gaza ni kuliangamiza kundi hilo na hatimaye kuwarejesha mateka na kuongeza kuwa malengo hayo yote yamo kwenye mpango huo ulioidhinishwa na ngazi za juu kabisa za serikali yake.