Pendekezo la waziri wa Italia kuwa na sarafu ya taifa badala ya Euro lakosolewa
7 Juni 2005Luxembourg:
Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro, wameupuuza wito wa kuachana na sarafu hiyo ya pamoja, baada ya waziri wa pili wa serikali ya Itali, kupendekeza kuundwa sarafu mpya ya taifa itakayofungamana na dola ya Marekani.Waziri mkuu wa Luxembourg Jean- Claude Juncker, alisema ni jambo la kushangaza na lisiloaminika kwamba nchi moja inaweza kujitoa katika sarafu ya Euro.Mzozo juu ya katiba ya Ulaya umesababisha msukosuko kwa sarafu ya Euro katika masoko ya fedha, ikishuka hadi kipimo cha Euro moja kwa dola 1.21 , baada ya matokeo ya kura ya maoni nchini Uholanzi juu ya katiba hiyo Jumatano iliopita.Wakati huo huo Mawaziri wa fedha wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro, wamefikiana kwamba yanapaswa kufikiwa makubaliano mnamo mwezi huu juu ya bajeti ya muda mrefu, ili kutoa hakikisho kwamba Ulaya bado inafanya kazi na ina uwezo wa kutoa maamuzi.