1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uvumi kuhusu umahamisho wa Ramos waendelea

27 Julai 2015

Beki wa Real Madrid Pepe amesema haingii akilini kwa timu hiyo kumpoteza mlinzi wake Sergio Ramos, huku kukiwa na uvumi kwamba Manchester United inajaribu kumvuta uwanjani Old Trafford

FIFA Klub-WM Real Madrid gegen San Lorenzo
Picha: Senna/AFP/Getty Images

Ramos amekuwa nahodha wa Los Blancos baada ya kuondoka kwa nahodha wa zamani na mlinda mlango Iker Casillas mapema mwezi huu.

Wakati huo huo Manchester United imepata saini ya mlinda mlango wa Argentina Sergio Romero katika mkataba utakaodumu kwa miaka mitatu.

Nae mchezaji wa kati wa Chile Arturo Vidal anakaribia kukamilisha hatua yake ya kuhama kutoka Juventus Turin kwenda Bayern Munich katika siku za karibuni baada ya kuwasili mjini Munich leo kwa ajili ya uchunguzi wa afya.

Mabingwa wa sasa wa Ulaya Barcelona na mabingwa wa premier league Chelsea , zikiwa katika maandalizi kwa ajili ya kutetea mataji yao, zinakutana kesho katika mchezo wa kirafiki mjini Washington.

Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amesema tathmini ya vipaji na majaribio ya nani anaweza kucheza na nani uwanjani ni muhimu kuliko kushinda, hata kama.

Mwandishi: Sekione Kitojo
Mhariri: Josephat Charo