Pezeshkian asema Iran itajikwamua dhidi ya vikwazo vyovyote
20 Septemba 2025
Matangazo
Katika matamshi yaliopeperushwa na shirika la habari la serikali, Pezeshkian amesema kupitia mchakato huo wa kuiwekea tena Iran vikwazo, mataifa ya magharibi yanafunga barabara lakini ni akili na mawazo yanayofungua au kujenga barabara.
Rais huyo pia amesema hawatasalimu amri chini ya shinikizo kwa sababu wana uwezo wa kubadilisha hali hiyo.
Mchakato huo utaweka tena vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran ikiwa makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia ya Iran hayatafikiwa kati ya Tehran na mataifa ya Ulaya yenye nguvu ndani ya wiki moja.