1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Pezeshkian: Iran haifikirii kuunda silaha za nyuklia

25 Septemba 2025

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kwamba nchi yake haina lengo la kuunda silaha za nyuklia.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa 2025 | Masud Peseschkian akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Rais wa Iran Masoud PezeshkianPicha: Kyle Mazza/CNP/picture alliance

Rais wa Iran Masoud Pezeshkian, amehutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kusema kwamba nchi yake haina lengo la kuunda silaha za nyuklia. Rais Pezeshkian ametoa hotuba hiyo wakati zikiwa zimebaki siku chache kabla ya vikwazo vya kimataifa kuanzishwa tena dhidi ya taifa hilo kutokana na shughuli zake za nyuklia.

Uingereza, Ufaransa na Ujerumani zimechukua hatua ya kurejesha vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambavyo vilikuwa vimesitishwa chini ya mkataba wa nyuklia wa 2015 ambao ulifikiwa na Marekani na kisha kuvunjwa na Rais Donald Trump. Wanadiplomasia wa pande mbili wamekutana kulijadili suala hilo kabla ya vikwazo vinavyotarajiwa kuanza jumamosi. Kiongozi huyo pia amelaani mashambulizi ya Israel na Marekani mnamo mwezi Juni akisema ni pigo kubwa kwa uaminifu wa kimataifa na matarajio ya amani ya kikanda.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW