1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pigo kwa Stuttgart, Guirassy nje kwa wiki kadhaa

23 Oktoba 2023

Serhou Guirassy anazidi kuweka rekodi katika Bundesliga kwa kufunga goli la 14 katika mechi 8 ila klabu yake ya Stuttgart yapata pigo kwa kuwa mshambuliaji huyo anatarajiwa kuwa nje kwa wiki kadhaa sasa.

 VfB Stuttgart vs. SV Darmstadt 98 |  Serhou Guirassy
Mshambuliaji wa VfB Stuttgart Serhou GuirassyPicha: Wolfgang Frank/Eibner/IMAGO

Mfungaji bora katika Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga kutoka klabu ya Stuttgart Serhou Guirassy atakuwa nje kwa wiki kadhaa baada ya kupata jeraha katika mechi yao ya mwishoni mwa wiki walipocheza na Union Berlin ambapo walipata ushindi wa 3-0.

Guirassy ambaye ni raia wa Guinea alifunga goli la kuvunja rekodi la 14 la msimu katika mechi nane za kwanza la Bundesliga, kabla kuondolewa uwanjani katika kipindi cha kwanza. Stuttgart hapo Jumapili ilitoa taarifa ikisema alipata jeraha dogo la paja lake la kushoto na atakuwa nje kwa wiki kadhaa.

Mshambuliaji huyo amepata sifa kutoka kila upande hata kutoka kwa kocha wa Bayern Munich thomas Tuchel.

"Kwa kweli ni mchezaji mzuri na timu yao iko kwenye msururu mzuri wa kupata matokeo. Kwa sasa wanashinda mara kwa mara na timu bila shaka inafunga magoli mengi," alisema Tuchel.

Chanzo: AFPE/Reuters

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW