Pinga vurugu za kijinsia na asilimia 77
24 Februari 2021DW, shirika la kimataifa la utangazaji la Ujerumani, na Asilimia 77, ambalo ni jukwaa lake kwa vijana wa Afrika, wanaungana na mwanamuziki wa Namibia, EES, katika kupigia chapuo kampeni ya mitandao ya kijamii itakayosaidia kuweka njia ya kupambana dhidi ya vurugu za kijinsia barani Afrika. Vidio ya muziki ya "Chooser" - wimbo uliotungwa na EES kwa kushirikiana na kipindi cha Asilimia 77 cha DW - imekwishatolewa. Kama hujauona, uangalie hapa chini:
Iwapo unaipenda vidio hii, unaalikwa kuungana nasi na kuonekana katika toleo maalumu mbadala litakalotolewa Machi 2121, likihusisha vipande vya vidio kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Pia utaingia katika droo ya kushinda moja ya spika tano za DW za "3-in-1" (ikijumuisha spika ya bluetooth + power bank + kipaza sauti)!
Hii ndiyo namna ya kushiriki:
- Rekodi vidio yako au mtu mwingine unayemfahamu akiimba au kucheza wimbo wa "Chooser." Unaweza kuimba au kucheza nao, unaweza kupiga makofi kufuatana na mdundo, unaweza kuonesha taarifa za uwezeshaji, matumaini au kupinga, au unaweza kutoa taarifa za kuona. Kuwa mbunifu, jukwaa ni lako!
- Vidio yako inapaswa kuwa na urefu usiopugua sekunde 15 - lakini isizidi dakika mbili.
- Tunapendekeza vidio yako uirekodi kwa mtindo wa mlalo (horizontal), lakini pia vidio za mraba (square) na wima (vertical) zitakubaliwa.
- Video zote zitumwe kwa njia ya barua-pepe kwenda 77@dw.com kabla ya Machi 14, 2021.
- Hakikisha unaweka anuani yako ya YouTube, Instagram, Twitter au jina la wasifu wa Tiktok ili tuweze kuwasiliana nawe.
- Tutachagua baadhi ya vidio hizi zionekane kwenye toleo mbadala la vidio ya muziki ya "Chooser" kwenye YouTube.
- Washindi watano wa spika za 3-in-1 watapatikana kupitia droo itakayochezwa Machi 24. Watumiaji wote waliotuma vidio watashiriki kwenye droo. Usijali hata usiposhirikishwa kwenye vidio - bado unaweza kupata zawadi!
- Kwa kututumia vidio, unairuhusu moja kwa moja Deutsche Welle (DW) na EES kutumia kuitumia vidio yako hiyo kwenye toleo mbadala la vidio ya "Chooser", na pia kwenye vidio zozote za matangazo zitakazotengenezwa makhsusi kwa kukuza ushirikiano huu wa kimuziki.
- Wafanyakazi wa DW hawaruhusiwi kushiriki.
- Vidio yako lazima ifuate miongozo ya kijamii ya YouTube na pia masharti ya ushiriki ya DW - vinginevyo itaondolewa. YouTube siyo mdhamini wa shindano hili, na haipaswi kuhusishwa kwa vyovyote na chochote kuhusiana nalo.
-Taarifa zozote za binafsi unazotoa kwetu zitatumiwa makhsusi kwa malengo ya shindano hili na hazitatolewa kwa watu au mashirika mengine bila idhini yako.
Unapambanaje dhidi ya vurugu za kijinsia katika maisha yako ya kila siku?
Hujui kuimba au kucheza? Hudhani kama unaonekana vizuri kwenye kamera? Tuna uhakika unaonekana vyema, lakini bado unaweza kushiriki katika shindano na kushinda mfuko wa wenye bidhaa za DW! Bonyeza tu kwenye kiunganishi cha vidio ya YouTube chini na ujibu swali kwenye sehemu ya maoni chini ya vidio:
Unapambanaje dhidi ya vurugu za kijinsia katika maisha yako ya kila siku?
- Machi 24, tutachagua majibu 15 bila kufuata utaratibu maalumu. Watumiaji hawa watashinda mfuko wenye bidhaa za DW. Kila zawadi inahusisha begi la mazoezi, barakoa na soketi ya pop.
- Ili kushinda, hakikisha umejisajili kwa chaneli yetu ya YouTube, DW Africa, wakati droo itakapofanyika.
- Tutawasiliana na washindi kupitia YouTube kwa kujibu maoni yao - hivyo kuwa makini kwenye kupokea ishara za kuingia kwa vidio mpya!
- Maoni hayatachaguliwa kwa kuzingatia maudhui ya jibu. Yatachaguliwa bila utaratibu maalumu.
- Maoni yenye matamshi ya chuki, taarifa za upotoshaji, uchafu au maudhui zozote zisizohusiana na swali la droo zitaondolewa.
- Wafanyakazi wa DW hawaruhusiwi kushiriki.
- Maoni yako lazima yafuate miongozo ya kijamii ya YouTube, pamoja na masharti ya ushiriki ya DW. Vinginevyo yataondolewa. YouTube siyo mdhamini wa shindano hili, na haipaswi kuhusishwa kwa vyovyote na chochote kuhusiana nalo.