1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kupeleka wanajeshi mpakani na Belarus

2 Agosti 2023

Poland imesema leo kuwa inawapeleka wanajeshi kwenye mpaka wake wa mashariki baada ya kuituhumu Belarus, mshirika wa karibu wa Urusi, kwamba helikopta zake za kijeshi ziliruka katika anga yake bila idhini.

Polen | Verlegung von Truppen an die polnisch-belarussische Grenze
Picha: 12 Brygada Zmechanizowana/Handout/REUTERS

WARSAW,

Jeshi la Belarus limekanusha ukiukaji wa aina hiyo na kuituhumu Poland ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, na ambayo ni moja ya waungaji mkono wa dhati wa Ukraine katika mzozo wake na Urusi, kwa kutunga tuhuma hizo ili kuhalalisha mkusanyiko wa askari wake mpakani. Wizara ya Ulinzi ya Poland imesema inatuma askari wa ziada na raslimali, zikiwemo helikopta za kivita. Imesema imeifahamisha NATO kuhusu ukiukwaji huo wa mpaka na kumuita balozi wa Belarus ili kutoa maelezo zaidi. Belarus imemruhusu Rais wa Urusi Vladmir Putin kuitumia mipaka yake kufanya mashambulizi nchini Ukraine, lakini Rais Alexander Lukashenko wa Belarus hajawapeleka wanajeshi wake katika vita hivyo.