Poland kuandaa kura ya maoni kuhusu sera ya uhamiaji Ulaya
13 Agosti 2023Matangazo
Waziri Mkuu Mateusz Morawiecki ametangaza swali litakaloulizwa katika kura hiyo ya maoni kupitia video iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Soma pia: Wahamiaji wanaotafuta ajira waongezeka Ulaya Mashariki
Limeonyesha kuwa chama chake cha Sheria na Haki, kinataka kutumia uhamiaji katika kampeni yake ya uchaguzi mkuu, mbinu ambayo ilikisaidia kuchukua madaraka mwaka wa 2015.
Serikali awali ilisema inataka kuandaa kura ya maoni pamoja na uchaguzi wa bunge unaopangwa Oktoba 15. Mawaziri wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya waliidhinisha mwezi Juni mpango wa kugawana jukumu la kuwahifadhi wahamiaji wanaoingia Ulaya bila vibali, suala ambalo ndio mzizi wa mojawapo ya mizozo ya kisiasa iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya jumuiya hiyo.