1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kuchukua kijiti cha Urais wa zamu wa EU mwakani

30 Desemba 2024

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk anatarajiwa kuchukua urais wa zamu wa Umoja wa Ulaya kutoka kwa Waziri Mkuu Hungary Viktor Orban Januari 1 mwakani, mabadiliko yamekuwa yanasuburiwa kwa hamu na mataifa mengi ya Ulaya.

Polen Donald Tusk
Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk anatarajiwa kuchukua urais wa zamu wa Umoja wa Ulaya kutoka kwa Rais wa Hungary.Picha: NATO

Poland ni miongoni mwa nchi zilizo msitari wa mbele katika kuiunga mkono Ukraine tangu ilipovamiwa na Urusi mwaka 2022, huku Hungary ambayo ni mshirika wa karibu wa Urusi  imekataa kuiunga mkono Ukraine. Mzozo wa Ukraine umekuwa ajenda kuu kwenye makao makuu ya Umoja huo mjini Brussels na mara kwa mara Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban amejikuta akizozana na viongozi wa Umoja wa Ulaya. Kwa muda mrefu, Poland na Hungary zimekuwa na uhusiano thabiti wa kitamaduni na kidiplomasia, lakini katika miaka ya hivi karibuni nchi hizo mbili za Ulaya zimetofautiana katika maswala kadhaa na kusababisha uhusiano wao kuzorota.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW