1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland yaiomba Marekani kuipa mitambo ya kinga dhidi ya makombora ya masafa mafupi kutoka Urusi

1 Februari 2008

WARSAW:

Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Poland amesema kuwa tisho la Urusi ni lazima lizingatiwe wakati nchi yake ikitafakari pendekezo kutoka Marekani,la kuweka mitambo ya kinga dhidi ya makombora ya masafa marefu nchini humo.Katika mazungumzo na maofisa wa Marekani wiki hii,waziri-Radek Sikorski- anatoa shinikizo la nchi yake kama fidia ya mapango huo ya kupewa msaada wa ulinzi kutoka Marekani.Maafisa wa Poland wamependekeza kuwa msaada huo lazima uwe katika aina ya mitambo ya ulinzi dhidi ya makombora ya masafa mafupi dhidi ya hujuma kutoka nchi jirani ikiwemo Urusi.

Urusi imetishia kuilenga tena Poland na makombora yake ya masafa marefu yenye vichwa vya Nuklia kujibu kile kinachoonekana kama jaribio la Marekani la kudumuza uwezo wa kijeshi wa Urusi.