Poland yapanga kusitisha kwa muda haki ya kuomba hifadhi
12 Oktoba 2024Poland imesema itajikita katika kukomesha uhamiaji haramu na kusitisha kwa muda haki ya kuomba hifadhi, kama sehemu ya mkakati mpya wa uhamiaji.
Akizungumza leo katika mkutano mkuu wa chama chake, Waziri Mkuu wa nchi hiyo Donald Tusk amesema atadai uamuzi huo utambuliwe Ulaya, ingawa hakutoa ufafanuzi zaidi. Kiongozi huyo wa Poland ameapa kupunguza uhamiaji haramu nchini humo hadi kiwango cha chini na amesema anapanga kuwasilisha mkakati mpya wa uhamiaji kwa baraza la mawaziri siku ya Jumanne.
Soma zaidi.Watunisia 12 wafa maji wakikimbilia Ulaya
Ameongeza kuwa, Poland inayopakana na Urusi na Belarus ambazo si wanachama wa Umoja wa Ulaya, inapaswa kurejesha udhibiti wa watu wanaoingia katika taifa hilo kwa asilimia 100.
Tusk amewatuhumu Rais wa Urusi Vladimir Putin na Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko kwa kuwaingiza wahamiaji mpakani kwa lengo la kuuvuruga umoja huo wenye mataifa 27 wanachama.