1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland yapinga mpango wa Marekani wa makombora ya ulinzi

5 Julai 2008

-

Waziri mkuu wa Poland Donald Tusk ameupinga mpango wa Marekani wa kutaka kujenga kambi ya kuweka makombora ya ulinzi katika ardhi ya Poland akisema serikali ya mjini Washington haitoi fidia ya kutosha kuhusiana na mpango huo.Waziri mkuu Tusk amewaambia waandishi wa habari kwamba kuwekwa kwa makombora hayo ya ulinzi ya Marekani katika ardhi ya Poland kutasababisha viitisho vipya nchini humo na kwahivyo mazungumzo zaidi yanahitajika kwa ajili ya kufikia makubaliano na Marekani katika suala la kuimarisha ulinzi katika anga ya Poland.Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imefahamisha kwamba mazungumzo na Poland yataendelea lakini hakuna maelezo zaidi yatakayotolewa kwa wakati huu.