1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Poland kuzungumza na Ukraine juu ya usafishaji nafaka

27 Septemba 2023

Poland imesema inafanya mazungumzo na Ukraine baada ya nchi hizo mbili kutumbukia kwenye msuguano, juu ya uamuzi wa serikali mjini Warsaw wa kurefusha marufuku ya usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia ardhi ya Poland.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: twitter.com/ZelenskyyUa

Hayo yameelezwa hii leo na waziri wa kilimo wa Poland Robert Telus muda mfupi baada ya kufanya mkutano na mwenzake wa Ukraine Mykola Solsky.

Telus ameyasifu mazungumzo hayo akiyataja kuwa njia muhimu ya kutatua tofauti zilizojitokeza kati ya nchi yake na Ukraine.

Soma pia:Makombora ya Urusi yamjeruhi mtu mmoja katika bandari ya Odessa nchini Ukraine

Mahusiano kati ya Ukraine na Poland yameingia doa baada ya Poland pamoja na nchi nyingine mbili za Umoja wa Ulaya za Hungray na Slovakia kuamua kurefusha marufuku ya usafirishaji nafaka za Ukraine kupitia ardhi zao. 

Uamuzi huo ulifikiwa kufuatia madai kwamba mazao ya Ukraine yaliyo njiani kwenda soko la kimataifa huuzwa kinyemela ndani ya mataifa hayo matatu na kuwaumiza wakulima wa ndani. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW