1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Poland yataka Ukraine ipatiwe makombora ya masafa marefu

3 Januari 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Radoslaw Sikorski amesema mataifa ya Magharibi yana jukumu la kuzidisha vikwazo dhidi ya Urusi na kuipatia Ukraine makombora ya masafa kujibu mashambulizi ya hivi karibuni ya Moscow.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Radoslaw Sikorski (kushoto) akiwa na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Radoslaw Sikorski (kushoto) akiwa na mwenzake wa Ukraine Dmytro Kuleba.Picha: UKRAINIAN FOREIGN MINISTRY/REUTERS

Sikorski amesema Ulaya inapaswa kujibu mashambulizi hayo ya Urusi kwa njia ambayo Rais Vladimir Putin anaielewa ya kumzidishia vikwazo vitakavyomzuia kutengeneza silaha zaidi.

Urusi imeendeleza mashambulizi makubwa ya makombora na ndege zisizo na rubani na kuilenga miji mbalimbali ya Ukraine, jambo lililoibua wito kwa mataifa ya Magharibi kutoa haraka msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine.

Aidha Urusi imefahamisha kuwa Kyiv imeushambulia kwa mara nyingine mji wake wa mpakani wa Belgorod ambao ulishuhudia pia mashambulizi makubwa siku ya Jumamosi yaliyosababisha vifo vya watu 25.