JamiiAfghanistan
Polisi Afghanistan yawakamata sita kwa kupiga muziki
2 Septemba 2023Matangazo
Afisa mmoja wa Taliban katika eneo hilo amesema kuwa watuhumiwa walikamatwa wakati wa sherehe ya kifamilia katika mji wa Mazar-e-Sharif.
Serikali ya Taliban liyorejea madarakani nchini Afghanistan mnamo Agosti 2021 imeweka marufuku kwa vyombo vya habari kupiga aina yoyote ya muziki .
Hivi karibuni, wamiliki wa kumbi za harusi nao waliagizwa kuepuka kupiga muziki. Taliban inauita uhamasishaji wa muziki kuwa ni aina ya ufisadi na kwamba, unasababisha "vijana kupotoka na uharibifu kwenye jamii."
Shughuli zinazopingana na sheria za Kiislamu zilipigwa pia marufuku katik harusi na matukio kama hayo. Kutokana na misimamo hiyo, wasanii wengi na wanamuziki wa Afghanistan wametafuta hifadhi katika mataifa ya Magharibi.