1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa wa ujangili akamatwa Afrika Kusini

14 Agosti 2024

Polisi nchini Afrika Kusini wamemkamata mshukiwa wa ujangili aliyekutwa na chaza mkavu mwenye thamani ya maelfu ya dola.

Chaza
Chaza mkavu mwenye thamani ya maelfu ya dola. Picha: Kim Kyung-Hoon/REUTERS

Nyama hiyo mara nyingi imekuwa ikisafirishwa kwa magendo kuelekea Asia. Mshukiwa huyo alikuwa na mabegi 27 ya plastiki yaliyokuwa na zaidi ya chaza elfu 13,000 wenye uzito wa kilo 640.

Wizara ya mazingira imetoa wito wa kufunguliwa mashtaka haraka dhidi ya mshukiwa huyo, ambaye alikamatwa wiki iliyopita. Mtu huyo alitiwa mbaroni wakati wa msako wa polisi huko Eastern Cape, mkoa wenye mwambao mrefu katika bahari ya Hindi.

Kilo moja ya chaza mkavu inaweza kuwa na thamani ya hadi randi 6,000 sawa na dola 330 za Kimarekani. Kiwango cha chaza kinachosafirishwa kimagendo kimeongezeka maradufu katika muongo mmoja uliopita, kulingana na mtandao wa ufuatiliaji wa biashara ya wanyamapori na viumbe wa baharini, TRAFFIC.