1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Polisi ahukumiwa maisha kwa kumuua mwanaharakati Iraq

8 Mei 2023

Polisi huko Iraq amekutwa na hatia na kuhukumiwa kifo kwa mauaji ya mchambuzi mashuhuri wa masuala ya usalama na mkosoaji wa mara kwa mara wa wanamgambo wenye nguvu.

Frauenrechte im Irak | Gerichtsgebäude in Bagdad
Picha: AHMAD AL-RUBAYE/AFP

Hukumu hiyo ya siku ya Jumapili, imetolewa katika kipindi cha  karibu miaka mitatu baada ya mchambuzi huyo kupigwa risasi nje ya nyumba yake Baghdad kufuatia vitisho vya wanamgambo.

Familia ya marehemu, Hisham al-Hashimi, imeonesha kufurahishwa na uamuzi huo, lakini pia imeonesha wasiwasi kwamba uenda ikabatilishwa na kukatiwa rufaa.

Al-Hashimi aliyekuwa na umri wa miaka  47, aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 2020 mbele ya nyumba yake huko Baghdad na washambuliaji wawili waliokuwa kwenye pikipiki baada ya kupewa vitisho kutoka wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW