1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Georgia yawakabili waandamanaji wanaoiunga mkono EU

29 Novemba 2024

Maelfu waliandamana katika mji mkuu wa Georgia na kwingineko siku ya Ijumaa, baada ya waziri mkuu Irakli Kobakhidze kutangaza kuchelewesha mchakato wa kujiunga na Umoja wa Ulaya na kukataa msaada wao wa kibajeti.

Georgia Tbilisi | Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Georgia
Mfuasi wa upinzani Georgia akiwakabilia maafisa wa polisi wakati wa maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa bunge mjini Tbilisi, Georgia.Picha: IMAGO/SNA

Polisi katika mji mkuu wa Georgia Tbilisi, wamekabiliana na waandamanaji usiku wa kuamkia leo, baada ya chama tawala cha Georgian Dream, kutangaza kusitisha mazungumzo ya kujiunga na Umoja wa Ulaya na kukataa msaada wa bajeti hadi mwaka 2028.

Soma piaBunge la Umoja wa Ulaya latoa wito wa uchaguzi mpya Georgia

Wizara ya mambo ya ndani ya nchi hiyo ilisema maafisa watatu wa polisi walijeruhiwa. Polisi walitumia maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakijaribu kuvunja lango la bunge.

Mahusiano kati ya Georgia na Umoja wa Ulaya yamezorota hivi karibuni, huku viongozi wa serikali wakiulaumu Umoja wa Ulaya kwa madai ya kujaribu kuchochea mapinduzi nchini humo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW