1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Polisi Kenya wafyatua risasi na mabomu kuzuia waandamanaji

7 Juni 2023

Polisi Kenya wamewalifyatulia gesi ya kutoa machozi na kuwakamata waandamanaji 11 walioandamana kupinga "muswada mpya wa fedha" wakosoaji wanadai muswada huo utapelekea matatizo ya kiuchumi kwa watu wa kawaida.

Kenia | Ausschreitungen und Proteste in Nairobi und Kisumi
Askari nchini Kenya akifyatua risasi kuwatawanya waandamanaji.Picha: Patrick Ngugi/AP Photo/picture alliance

Polisi jijini Nairobi walifyatua risasi kadhaa na mabomu ya machozi na kuwakamata watu 11 kisha kuwatia kwenye lori la polisi ili kutawanya maandamano hayo.

"Shusha muswada wa fedha" waandamaji waliimba huku kundi la takribani watu 100 wakiandamana kuelekea bungeni ambalo limeanza tena Jumanne baada ya mapumziko na linatarajia kujadili sheria hiyo wiki hii.

Maandamano hayo yaliyopewa jina la sita sita yaliyofanyika siku ya sita ya mwezi wa sita huku waandamanaji wakiwa na mabango yaliyoandikwa "Je, kodi itashusha gharama za maisha" na mengine "Umasikini ni wa kutengenezwa na binadamu."

 "Tunafukuzwa lakini tunapigania haki zetu" alisema mmoja wa waandamanaji Rogers Obogi kijana asiye na kazi mwenye umri wa miaka 23. Tunaandamana ili kueleza masikitiko yetu, watu wanahitaji pesa, pesa hizo zinatozwa kodi mara mbili, watu wanahitaji pesa hizo fedha zinatozwa ushuru mara mbili"

Soma pia: Polisi washutumiwa kwa mauaji Kenya.

Amnesty ilitoa wito wa kuachiliwa bila masharti watu 11 waliokamatwa ikisema haki ya kuandamana, kujieleza na kushiriki katika mazungumzo ya hadhara ni chini ya katiba na sheria ya kimataifa.

Naye mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi alilaani kukamatwa kwa watu hao huku akiandika katika mtandao wa Twitter "kutuma polisi kwenda kukamata waandamanaji wa amani huku wakitimiza haki yako ya kusikilizwa ni tabia ya udikteta.

"Hakuna maandamano ya amani yanayolenga mazungumzo ya uchumi ya kitaifa yanayoendelea yanapaswa kukatizwa na kukamatwa kwa mtu yoyote" alisema Korir Sing´oei Katibu mkuu wa Wizara ya mambo ya nje.

Rais William Ruto anataka kuuimarisha uchumi ulio na madeni yaliyorithiwa kutoka kwa mtangulizi wake Uhuru Kenyatta ambae alitumia miradi mikubwa ya miundo mbinu.

Serikali yakosolewa kwa ongezeko la mishahara kwenye bajeti ijayo

Raia waandamanaji wakikabiliana na polisi mjini Nairobi.Picha: Gerald Anderson/AA/picture alliance

Serikali yake imetayarisha bajeti ya shilingi trilioni 3.6 kwa mwaka 2023/2024 huku mapendekezo mapya yakitarajiwa kuanzisha shilingi bilioni 289 wakosoaji wanamshutumu Ruto kwa kurudisha makasia ahadi alizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Agosti 2022 alipojitangaza bingwa wa wakenya masikini na kuahidi kuboresha hali ya uchumi.

Chama cha Azimio cha Raila Odinga kimeukosoa muswada huo kikisema serikali ya Ruto ilitaka kuchukua mabilioni kutoka mifukoni mwa watu masikini zaidi katika nchi hii huku wakitaraji kushangilia "Tumekataa kuketi na kutazama wakenya wakinyanyasika ili kurekebisha uhaba wa fedha uliosababishwa na usimamizi mbovu, ufujaji wa fedha, ufisadi na kuajiriwa kwa nyadhifa muhimu za umma. Azimio ilisema katika taarifa yake ya Mei 30.

Soma pia:Polisi Kenya watawanya maandamno dhidi ya mswada wa fedha 

Odinga mapema mwaka huu aliongoza msururu wa maandamano kuhusu mgogoro wa gharama za maisha nchini Kenya na malalamiko yake kwamba hakutendewa haki katika uchaguzi wa urais.

Mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu Amnesty International lililo na makao yake mjini London na Human Rights Watch lililo na makao yake mjini New York, yalisema katika ripoti ya wiki iliyopita kwamba watu 12 waliuawa na polisi katika maandamano mwezi Machi huku takwimu za serikali zikiainisha kuwa ni watu 3 ndio waliouawa akiwemo askari polisi.